Saturday 16 March 2013

MIKE "SONKO" MBUVI YUKO KWA "YOKI "

       Yoki ni "ijoki" sina jina lake kamili lakini utumiwa kufungia Ng'ombe ili ikokote gari la Ng'ombe "ikasya"

      Basi Sonko munakumbuka kesi nyongi sana zilimuandama?Hii ilikua ana pewa misukasuko hio ili awe mmoja wao.

      Sote twajua Kenya imekua kwa mikono ya watu fulani,ivyo wao wakikutaka uwa wanakupa misukasuko ili usalimu amri

      Mtu anasema ushikwe ili aje kukutoa ndio umuone kua mzuri wako na niyeye alie tumana ushikwe.

Msishangae kumuona Sonko yuko upande huo aliopo,

   Apa wanataka kumuingiza Johnstone Muthama,Ubaya wetu wakenya atusaidii mtu anapo banwa ni sisi kuwasaIDI

Uchaguzi wa Urais ulikua vurugu mechi

        Uchaguzi wa Urais ulingia dosari nyingi sana,Kenya twaelewa kupiga kura ni haki ya kila mkenya na Kenya chini ya hii katiba mupya kila mtu ana haki yake ya musingi.

        Habari nilinzo pata vuvuzela,fujo na balaa ilitokea 3am 4 march 2013,Watu Githurai nanasikia ni kwote sehemu za Uhuru watu walipigiwa makelele wamuke wende kupiga kura.
  
       Na ilipo fika 11am 4 march 2013 basi kila mtu alilazimishwa kuonyesha kidole kama amepiga kura na ukikutikana una wino wakupiga kura basi biashara yako ili haribiwa kabisa.

   JE IEBC ILIENDESHA UCHAGUZI KWA NJIA YA HAKI?IWAPO WATU WALILAZIMISHWA KUPIGA KURA.

     Nawengine wakapoteza maisha,hii ilifanywa Pwani kutishia watu wasijitokeze kwa wingi kwakua ni sehemu iliojulikana kua  ni sehemu ya Raila,apa kila kitu kilipangwa kikapagika kwa vikao vyao vingi tu walivyo vikaa kabla ya uchaguzi.

    IEBC NI TUME AMBAYO ILITEGEMEWA KUA ITAENDESHA UPIGAJI WA KURA KWA NJIA YA HAKI NA UWAZI,UCHAGUZI HUU AUKUWA WA HAKI NA UWAZI KATAA KUBALI

MSIKUBALI KUTUMIWA KUKWAMISHA JUHUDI ZA MASINI WENZETU KUJIKOMBOA

      Kila kitu kiko wazi apa hizi ni juhudi za wachache walio nacho kupinga hali ya mkenya masikini,Nina hakika wenzetu wako mbele kwa kutanguliza pesa.

     Laikini sisi mshikamano wetu utatukomboa,Tuwe wajanja nakuchambua juhudi yeyote

Hon Johnstone Muthama kusema ni haki yake ya msingi na haiwezekani yeye kutishiwa maisha wakuongea ukweli.

     Mkae mjue kuna vitisho vingi kila mahali ata PS's wanatumiwa lakini musi hofu kuongea ukweli si ku "hate speech" matamushi ya chuki nikusema piga,ondoa lakini ukweli hauwezi ata siku moja ukageuka kua "hate speech"

Wakenya tujiandae kwa maandamano ya "AMANI"

      Mandamano si uvunjaji wa amani bali ni njia moja ya kuonyesha kutoridhishwa ni mamuzi fulani au mambo yanavyo endeshwa.

       Tunajua kuwa kuna kundi ambalo limekua likifaidika ni uwongozi ulioko Afrika,kwakua mambo yao yanawaendea.

       Ebu geuka apo ulipo na uangalie au ukumbuke vitu vilivyo kua tulipo pata uhuru 1963 na sasa

1;Mabasi ya kutoa huduma "KBS" hayaikua hivi,kuna watu ambao kazi yao ni kuiba na kufilisi ili wawe na biashara hio.
Matatu ndio zime wekwa ili kukinyesha nauli zina pandishwa na kukiwa na sikukuu au chochote kile

2;Sipitali zimekua aziendeki zile za umma madawa zinahamishwa kwakupelekwa kwa za binafsi,
3;Watu wamekua wanyakuzi wa chochote cha umma
4;Gari la moshi kama mukumbukavyo walikua wakitoa huduma mara 4 kwa siku "train "ya Mombasa ambayo ilikua ikiondoka 6pm na 7pm Mengine 2 Kisumu kila siku bila ya kuchelewa,Yako wapi leo?
5;Bandari wanaimezea mate hao hao ndio wanaiba alafu wasema Bndari aileti faida

Friday 15 March 2013

ATUPENDI KUSEMEWA

      Kuna watu ambao midomo yao utumika kufunika ukweli,Musiwe muna kimya mtu kuwasemea alichopewa ale pekeyake,Ukombozi Kenya watakiwa tunganishe nguvu.

     NGO's,Vikundi fulani au watu wanao jiita hivi au vile wakienda kwa vyombo vya habari FM Radio's,TV na magazeti wanatumika kufunika uwonzo wa kupora haki yetu apa Kenya

YAPO MAELEZO UPO USHAHIDI WALIOTOA MAGIZO

     Yapo maelekezo kua mtu fulani apa kwetu Kenya asitawale,Niwazi nguvu ya aina yoyote ili muradi mtu X na Y asiwai tawala.

     Yapo maelezo upo ushahidi waliotoa maginzo

Wangombea X X atuwataki.

Kuna watu amboa utengenezwa kuharibu au walio tengenezwa waweke pingamizi wapo munawajua vizuri sana mfano hai ni Livondo au Tuju,Mudavadi,Kenneth na group yote ilimuradi Raila Amollo asiwe Rais apa kenya hali hii nituipinge kwa nguvu yote 

KULIKUA NA TARIFA ZA KIMAPEMA KUA KURA ZITABADILISHWA ZIWE ZA JUBILEE UKO VITUONI VYA KUPIGA KURA

        Kulikua na tarifa za awali kua Jubilee walipanga kuwanunua baadhi ya mawakala wa CORD na kubadilisha kura masandukuni kwa baadhi ya sehemu na kukukwamisha baadhi ya sehemu.
   
Nyote mulishuhudia kura za Uhuru sehemu alikua akipata zaidi ya  70,000 au 90,000 na sehemu zake Raila akishinda ulisikia 30,000 au 20,000 huu ni mpango ulio sukwa ni wakuu kando ya pazia mkuu wao akiwa Moi ndio maana walikwamisha mitambo kimakusudi ili warudi kwa zama zake.